Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro  amesema hawezi kuzungumzia tuhuma  za kukamatwa kwa Mkurugenzi wa Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo, huku akiwatoa hofu waandishi wa Habari juu ya kauli ya Mzee wa Upako

Sirro amesema kuwa tuhuma za kukamatwa kwa Mkurugenzi wa Jamii Forum na kushikiliwa na Jeshi la Polisi atazitolea ufafanuzi ijumaa ya wiki hii.

Aidha, Sirro amewatoa hofu waandishi wa habari kuhusu kauli ya Mchungaji wa kanisa la Maombezi (GRC ) Ubungo kibangu, Anthony Lusekelo kuwa waandishi waliomwandika vibaya watakufa, Sirro amesema kauli hiyo  inaweza kumpa hofu mpagani pekee.

“Kwa hiyo mpagani  akisikia ya mtu mwingine mpagani kwa sababu anafikiria upgani wake, ataanza kuwa na wasi wasi, lakini kwa sababu unajua Mungu ni huyu mmoja, na yeye ndiye aliyekuleta duniani pia ndiye atakaye kutoa duniani, hupaswi kuwa na hofu”amesema Sirro.

JPM afyeka 230 NEC, 10 Kamati Kuu CCM
Lowassa adai TB Joshua amemtabiria urais 2020