Mwenyekiti wa Kampuni ya kutengeneza magari ya Nissan, Carlos Ghosn amekamatwa kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha.

Taarifa iliyotolewa leo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Hiroto Saikawa imeeleza kuwa pamoja na kutiwa mbaroni, Ghosn atafukuzwa rasmi kazi baada ya kikao cha Bodi ya Wakurugenzi kitakachofanyika Alhamisi wiki hii.

Anatuhumiwa kwa kufanya ubadhirifu mkubwa wa fedha ikiwa ni pamoja na kudanganya kuhusu fedha anazolipwa na kutumia mali ya kampuni kwa matumizi binafsi.

Mwendesha mashtaka wa Serikali ya Japan hajazungumzia kukamatwa kwa Ghosn, aliyekuwa anaiongoza kampuni hiyo inayoshika nafasi ya sita kwa utengenezaji na uuzaji wa magari duniani.

“Ninasikia kukasirishwa na kushushiwa heshima. Naamini kadiri habari hii inavyozidi kuwekwa wazi watu wengine pia watajisikia kama ninavyojisikia leo,” aliongeza.

Saikawa amewatoa hofu wadau wa kampuni hiyo, akieleza kuwa wanafanya kila liwezekanalo kuweka sawa hali iliyopo na kurejea katika oparesheni za kila siku kwa ajili ya manufaa ya wafanyakazi, wateja na washirika wake.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 20, 2018
Wawekezaji kutoka Uturuki watua nchini

Comments

comments