Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka watanzania kupuuza taarifa zinazodai  noti ya 500, haitatumika kuanzia Desemba 31 mwaka huu kama inavyovumisha kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi  wa Huduma za Kibenki wa BoT, Mercian Kobello, katika kukanusha  uvumi huo, amesema taarifa zilizozagaa kuwapo kwa kikomo cha matumizi ya noti ya sh. 500 mwishoni mwa mwaka huu sio za kweli.

“Benki kuu ya Tanzania inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa habari inayoenea katika mitandao mbali mbali ya kijamii kwamba noti ya shilingi mia tano haitatumika tena kuanzia Desemba 31,2016 siyo taarifa ya kweli na ni uvumi unaopaswa kupuuzwa”amesema Kobello.

Aidha ameongeza kuwa ukweli wa noti ya shilingi mia tano itaendelea kutumika katika mzunguko sambamba na ile sarafu ya shilingi 500 hadi pale noti hiyo itakapotoweka mikononi mwa wananchi.

Taarifa kuhusu noti ya 500 kutotumika tena  ifikapo jumamos, zilizagaa katika mitandao ya kijamii tangu juzi na kuibua wasiwasi miongoni mwa wananchi waliokuwa na noti hizo.

Jaffo atoa onyo kwa wakurugenzi na makandarasi
Polisi wazuiwa kuwavisha mabango madereva wanaokiuka sheria barabarani