Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imehamishia mali na madeni yote ya Bank M kwenda Azania Bank baada ya benki hiyo kushindwa kuwahudumia wateja wake pamoja na kulipa madeni yao.

Akitangaza taarifa, Naibu Gavana Dk. Bernad Kibese amesema kwamba baada ya kutafuta njia mbalimbali za ufumbuzi wa matatizo ya Benk M, muafaka uliopatikana ni kuhamisha mali zote kwenda Benki ya Azania Bank Limited kwa mujibu wa sheria.

Aidha Dk. Kibese ameeleza kwamba wateja wenye mikopo wametakiwa kuendelea kulipa mikopo yao kulingana na mikataba yao huku benki kuu ikiahidi kufuatilia suala hili kwa ukaribu zaidi.

Aidha Dk Kibese amewatoa wasiwasi wateja wanaohamishiwa Azania Bank, kwamba Benki hiyo inatarajia kuwa na mtaji wa shilingi bilioni 164, ambayo ni kiwango cha juu cha mtaji unatakiwa kuendesha shughuli za kibenki ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 15 hivyo itaweza kuhudumia wateja wake wa zamani na wapya.

Benki kuu itaendelea kulinda maslahi ya wateja wa huduma za kibenki na kuimarisha uhimilivu wa sekta ya fedha nchini.

“Benki inapoonekana kutetereka lazima Beki Kuu inaingilia kati na inaingilia kati ili kulinda amana ya wateja”, amesema Dk. Kibese.

 

Breaking: Magaidi wavamia hoteli Nairobi, wafyatua risasi na mabomu
Masauni atoa onyo 'Msithubutu kuwaazimisha silaha wahalifu'