Serikali nchini Ugiriki imesema inafanya opresheni kubwa ya uokozi kusini mwa kisiwa cha bahari ya Mediterania cha Crete kuwaokoa mamia ya wahamiaji waliomo ndani ya boti iliyopotea na kujikuta kwenye eneo la bahari lenye mawimbi makubwa.

Aidha, walinzi wa pwani ya Ugiriki wamesema abiria kwenye boti hiyo inayoaminika kuwa imewabeba kati ya wahamiaji 400 hadi 500 ndiyo walituma ujumbe wa kuomba msaada usiku wa kuamkia leo kwa kutumia namba ya dharura.

Boti ya Polisi katika Uokozi.

Mamlaka hiyo imesema, Meli kadhaa ikiwemo mbili za wavuvi wa Italia zinashiriki zoezi la kuwaokoa wahamiaji hao lakini hali mbaya ya hewa kwenye eneo la bahari limefanya operesheni hiyo kuwa ngumu na hadi sasa hakuna mtu aliyookolewa.

Hata hivyo, bado hijafahamika hadi sasa eneo ambalo boti hiyo iling´oa nanga au ilipokuwa inaelekea na maafisa bado hawajatambua uraia wa abiria waliomo ndani ya chombo hicho.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 23, 2022 
Sergio Busquets bado yupo yupo Hispania