Nchi ya Botswana  inamlaumu Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, Joseph Kabila kwa matatizo ya kibinadamu na usalama yanayoendelea nchini humo.

Wamesema yawezekana matatizo hayo yanatokana na Rais, Kabila kung’ang’ania madaraka na kukataa kwake kujiuzulu.

Mataifa ya magharibi yamerudia mara kwa mara kumkosoa Kabila ambaye muhula wake wa kuwa madarakani uliisha tangu Disemba mwaka 2016 lakini mataifa ya kiafrika yanachukulia suala hilo taratibu wakipendekeza utaratibu kuelekea uchaguzi uliocheleweshwa kwa muda mrefu lakini wanaepuka kumlaumu moja kwa moja Kabila.

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ilijikomboa mwaka 2003 kutoka vita vya miaka mitano ambavyo mamilioni ya watu walikimbia nchi hiyo na mamilioni kuuliwa, wengi kutokana na njaa pamoja na magonjwa, na mzozo wa kisiasa uliopo hivi sasa umechangia mgogoro mkubwa ambao umewalazimisha mamilioni ya watu kukimbia nyumba zao.

Watu 22 wakiwemo raia 15 waliuwawa katika siku mbili zilizopita katika mapambano ya kikabila huko mashariki mwa Congo katika jimbo la Kivu kaskazini, ofisa mmoja alisema.

IGP Sirro awanyooshea kidole wanaopanga maandamano nchi nzima
Kamanda Mambosasa: Kitakacho wakuta tusilaumiane