Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita, emechaguliwa tena kuwa rais baada ya kushinda kwenye duru ya pili ya uchaguzi na kumshinda mpinzani wake, Soumaila Cisse

Kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyotangazwa na wizara ya mambo ndani, Keita mwenye umri wa miaka 67 amepata asilimia 67.17 ya kura zilizopigwa Jumapili iliyopita, huku mpinzani wake, Cisse akiwa amepata asilimia 32.83. Asilimia 34.5 ya watu ndiyo walijitokeza kupiga kura. Cisse, mwenye umri wa miaka 68 na waziri wa zamani wa fedha pia aligombea urais dhidi ya Keita mwaka 2013.

Aidha, Chama cha Cisse kimeapa kuyapinga matokeo hayo kwa kutumia njia za kidemokrasia, ambapo siku ya Jumatatu, Cisse alitangaza kwamba atayapinga matokeo na kuwataka wananchi wa Mali kusimama pamoja kupinga udikteta wa udanganyifu.

Hata hivyo, uchaguzi huo uligubikwa na mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa jihadi, hatua iliyolazimu kufungwa kwa vituo vya kupigia kura vyenye watu wachache.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Agosti 17, 2018
Atupwa jela miaka mitano kwa wizi wa zaidi ya mil. 9