Muigizaji gwiji, Brad Pitt ameweka wazi hali yake ya kiakili na kimaisha baada ya kuvunjika kwa ndoa yake na mwigizaji mwenzake, Angelina Jolie.

Katika mahojiano aliyofanya na shirika la habari la Associated Press, Pitt alisema kuwa kilichomtokea kilikuwa changamoto kubwa kwenye maisha yake lakini inabidi kizungumziwe tu bila usiri kwakuwa amebaini kuwa hali ya ubinadamu ina mvuto wake.

Akizungumzia kama alifikia hatua ya kutaka kujitoa roho kutokana na uamuzi wa staa huyo wa ‘Maleficent’, alidai kuwa yeye sio mtu wa kujitoa mhanga.

“Mimi sio mtu wa kujitoa mhanga au kitu chochote. Bado kuna vitu vizuri kwenye hii dunia na mapenzi tele. Na kuna mapenzi tele ya kutoa. Yote sawa, ni maisha tu,” alisema Pitt.

Kulikuwa na taarifa kuwa baada ya kuvunjika kwa ndoa yao, Pitt alichanganyikiwa kiasi cha kuhudhuria matibabu maalum ya kisaikolojia (rehab).

Brad Pitt ambaye ni baba wa Maddox (15), Pax (13), Zahara (12), Shiloh (10) na mapacha Vivienne na Knox (8) alisema kuwa wawili hao wamekubaliana njia bora zaidi ya kuendelea kuwaangalia watoto kwakuwa watoto ni kipaumbele cha kwanza.

Wawili hao waliachana baada ya miaka 12 ya uhusiano wao ambapo Angelina alidai Pitt amemsaliti. Walianza uhusiano wao siku kadhaa baada ya kukamilisha kurekodi filamu yao iliyotamba ya ‘Mr & Mrs. Smith’.

Toto waahidi kulitoa tone la mwisho Kuikaba Yanga Wasishuke
Mwandishi Mahiri wa Habari za Dawa za Kulevya auawa kwa Risasi