Habari za hivi punde ni kwamba mfanyabiashara maarufu nchini na muwekezaji klabu ya Simba, Mo Dewji mapema asubuhi ya leo ametekwa na watu wasiojulikana.
Tukio hilo limetokea mapema leo wakati akielekea hoteli ya Colosseum kwa ajili kufanya mazoezi (gym) ambapo watu hao wasiojulikana walifyatua risasi hewani na kuondoka nae.
 
Kamanda wa polisi Kinondoni Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Aidha RPC Lazaro Mambosasa amesema Polisi Dar inafuatilia tukio hilo la lutekwa kwa mfanyabiashara huyo mkubwa hapa nchini.
Al-Shabab watangaza kuwaua wapelelezi wa Marekani, Uingereza
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 11, 2018

Comments

comments