Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kusitisha maandamano na mikutano nchi nzima iliyokuwa imepangwa kufanyika kesho (Septemba 1) waliodai ni uzinduzi wa Oparesheni ya kile walichokiita Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA).

Chadema wamesema wameahirisha UKUTA kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo ili kutoa nafasi ya mazungumzo iliyoombwa na wadau na viongozi wa dini nchini.

Akizungumza muda mfupi uliopita na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na viongozi wa dini kuwapa angalau wiki tatu.

“Viongozi wa dini walituambia tupeni wiki mbili au tatu, sisi tukawaongeza nyingine moja,” amesema Mbowe na kuongeza kuwa chama hicho kimepata wakati mgumu kufikia uamuzi huo baada ya wadau mbalimbali kuwasihi kutofanya maandamano, badala yake watoe nafasi ya kuzungumza na Serikali ili kufikia muafaka kwa amani.

 

Moussa Sissoko Arejea England, Spurs Wahusishwa
Serikali yamjibu Kitwanga, yatetea ununuzi wa ndege za Bomberdier Q400