Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewakumu kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya shilingi milioni 5 kila mmoja, aliyekuwa waziri wa zamani wa fedha, Bazil Mramba na aliyekuwa waziri wa madini na nishati, Daniel Yona.

Mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo baada ya kuwakuta na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisabishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11. 7.

Hata hivyo, mahakama hiyo imemuachia huru aliyekuwa katibu wa wizara ya fedha, Gray Mgonja aliyekuwa mmoja kati ya washitakiwa katika kesi hiyo.

Vijana Wa Obama Wawaliza Wajapan Kombe la Dunia
Silaha Za Azam Toka Ughaibuni Zajiandaa na Kagame Cup