Hatimaye uhasama uliodumu kwa muda mrefu kati ya Lady Jay Dee na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba umeripotiwa kufika tamati baada ya mwimbaji huyo kukubali ombi la kuyamaliza.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Millard Ayo, uongozi wa Komando Jide umuandikia ujumbe leo na kumueleza kuwa yaliyopita sasa yamefikia tamati na kwamba kituo hicho cha kinaweza kuendelea kupiga nyimbo za Jide.

Uamuzi huo wa uongozi wa Jide umekuja ikiwa ni siku chache baada ya Ruge kueleza kupitia XXL ya Clouds Fm kuwa hawana matatizo yoyote na mwimbaji huyo na kwamba wanachosubiri ni agizo kutoka kwake waanze kucheza nyimbo zake.

Ruge pamoja na mmiliki wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga walikuwa na mtafaruku na mwimbaji huyo uliopelekea kufungua kesi mahakamani. Wawili hao walimshtaki Jide kwa kutolea maneno ya kashfa kwenye mitandao ya kijamii ambapo mahakama ilimkuta na hatia na kumuamuru kuwaomba radhi kupitia vyombo vya habari.

Video: Mbowe taabani kifedha, Sakata la Dangote kaa la moto...
TPDC: Kampuni ya Dangote wamepotosha umma