Habari njema kutoka katika eneo la mapambano kati ya Jeshi la Polisi na majambazi, eneo la Vikindu, Mkuranga mkoa wa Pwani zinaeleza kuwa jeshi la polisi limefanikiwa kuwazimisha majambazi hao.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa majambazi wote ambao idadi yao haijajulikana wameuawa na Polisi wameanza kuondoka katika eneo hilo.

Hata hivyo, Jamii Forums wameripoti kuwa askari mmoja wa Jeshi la Polisi ameuawa kwa kupigwa risasi katika mapambano hayo.

Mapambano kati ya Jeshi la Polisi na Majambazi hayo yalianza usiku wa manane na kumalizika muda mfupi uliopita, ambapo magari zaidi ya 16 ya Jeshi la polisi yaliyokuwa yameelekea katika eneo la tukio yameonekana yakirudi baada ya kukamilisha kazi.

Endelea kufuatilia Dar24 kupata tamko rasmi la Jeshi la Polisi kuhusu tukio hilo.

Audio: Makonda atoa wito kwa Haki za Binaadamu, awataka kulaani mauaji ya Polisi Dar
Polisi wapambana na Majambazi, mapambano yaendelea Mkuranga