Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu ametangaza kisa cha kwanza cha mgonjwa wa virusi vya corona ambaye ameingia nchini jana Machi 15 2020 kutoka Ubeligiji.

Akitangaza kisa hicho, amewatoa hofu wananchi kwa kuwa mgonjwa huyo ametokea nje ya nchi hivyo uwepo wa maambukizi kwa watu wengine ndani ya nchi ni mdogo.

“Jana tarehe 15 Machi 2020, tulipokea msafiri mtanzania mwanamke mwenye umri wa miaka 46 ambaye aliwasili nchini na  ndege ya Rwand Air akitokea nchini ubeligiji”.

Iran: Mjumbe wa baraza kuu la kidini afariki kwa corona

“Msaifiri huyu aliondoka nchini Machi  3, 2020 ambapo kati ya tarehe 5 mpaka 13 Machi alitembelea nchi za Sweeden na Denmark na kurudi tena Ubeligiji na kurejea machi 15 saa kumi jioni” Ameeleza Waziri Ummy

Waziri Ummy ametoa pongezi kwa mgonjwa huyo kwa hatua alizochukua baada ya kuingia nchini na kujipeleka mwenyewe hospitali.

“Mgonjwa huyo kwa sasa yupo Arusha, na alipofika nchini na kuona anakohoa aliingia hotelini na kujifungia kisha akafika hospitali ya Mawenzi kwa vipimo. Saa saba usiku tulipokea sampuli na watu wa maabala wamethibitisha kuwa mtu huyu ana maambukizi ya virusi vya corona”.

Magufuli asitisha mbio za mwenge kuepusha Corona

Waziri Ummy amesema wizara imejiandaa vizuri kwa vifaa na mafunzo kwa wauguzi, na iliangalia sana mikoa yenye viwanja vikubwa vya ndege ambayo tayari kuna vituo vya kuwatenga wagonjwa watakao kutwa na maambukizi.

Hadi kufikia alfajiri ya leo, Watu 169,605 walikuwa wameambukizwa virusi hivyo huku Watu 6,518 wakipoteza maisha na Watu 77,775 wakipona.

Video: Chadema yatangaza mikutano ya hadhara nchi nzima
FIGC waomba EURO 2020 iahirishwe