Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa jumla ya watu 11 wamefariki Dunia wakiwemo waandishi wa habari watano baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana na gari dogo aina ya Hiace

Waandishi hao walikuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakielekea Ukerewe kwenye ziara maalumu ya kikazi

Akizungumza na Dar 24 Media Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Blasius Chatanda amethibitisha kutokea ajali hiyo na kutaja chanzo cha awali cha ajali hiyo kuwa ni mwendokasi

Kamanda Chatanda amesema taarifa zaidi za hali za majeruhi na idadi ya vifo vitakavyoongezeka zitatolewa baadae baada ya tathimini na uchunguzi wa kitabibu

Ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Januari 11 katika eneo la Nyashomi.

Endelea kufuatilia Dar 24 Media tutaendelea kukupa taarifa zaidi.

Rais Samia awalilia 14 waliofariki ajali ya gari Mkoani Simiyu
Kiongozi wa kiraia Myanmar kufungwa jela miaka minne