Ajali mbaya imetokea katika mlima Rhotia kabla ya kuingia wilayani Karatu mkoani Arusha baada ya basi lililokuwa limemeba wanafunzi wa shule ya msingi ya Lucky Vicent waliokuwa wanaenda kufanya mashindano ya ujirani mwema Karatu kutumbukia kwenye korongo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, bali hilo lilikuwa limebeba wanafunzi wa darasa la saba zaidi ya 40 ambapo zaidi ya watu 32 wamepoteza maisha, kati yao ni Wavulana 12, Wasichana 17, pamoja na walimu 3 na majeruhi 3 ambao hali zao ni mbaya na wamewahishwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo athibitisha na kusema punde atatoa taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo.

?Live: Kamanda Mkumbo akizungumzia ajali mbaya iliyotokea Arusha
Video: Sugu ang'aka bungeni wanasiasa kuwatumia vibaya wasanii

Comments

comments