Askari wawili wa kikosi cha usalama barabarani wa wilayani Kibiti wameuawa baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika kijiji cha Msafiri, kata ya Bungu wakiwa kazini.

Pia watu hao wamechoma moto gari moja na Pikipiki za askari hapo kisha kutoweka kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi Mikoani Pwani, Onesmo Lyanga amethibitisha kutoka kwa tukio hilo.

Tukio hili limetokea kilomita chache kutoka eneo ambalo waliuawa askari Polisi wanne kwa kupigwa risasi katika eneo la Mkengeni walipokuwa wakitoka doria katika kijiji cha Jaribu

RC Mghwira ashindilia msumari shamba la Mbowe kuondolewa miundombinu
Video: CUF wamaliza mgogoro wao, wapata bodi mpya inayotambuliwa na msajili