Bunge la Uingereza leo limeukataa rasmi mkataba wa Waziri Mkuu, Theresa May kuhusu kujitoa kwa nchi hiyo katika Umoja wa Ulaya (Brexit), ikiwa zimebaki siku chache tu nchi hiyo ijiondoe.

Wabunge 391 wamepiga kura kuukataa mpango wa mkataba wa Waziri Mkuu huyo wenye mkakati maalum kuhusu Brexit, huku wabunge 242 wakipiga kura ya kumuunga mkono.

Uingereza inatarajia kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya Machi 29 mwaka huu majira ya saa tano usiku, kwa kuzingatia mawazo ya walio wengi kupitia kura ya maoni. Juni 2016, asilimia 51.9 Uingereza ilipiga kura ya maoni kuunga mkono Brexit hatua ambayo ilikuwa pigo la kwanza kwa Waziri Mkuu huyo ambaye alikuwa akiwashawishi kutounga mkono kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Uamuzi huo wa Bunge umepokewa kwa hisia tofauti na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo. Waziri Mkuu wa Hispania, Pedro Sanchez alionesha kutounga mkono kupitia mtandao wa Twitter akisema, “tuilinde Ulaya yetu na Ulaya itulinde.”

Wengine walioonesha kusikitishwa na uamuzi huo ni Waziri Mkuu wa Uholanzi, Mark Rutte na Waziri Mkuu wa Denmark ambaye ameandika kwenye Twitter, “inasikitisha.”

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Machi 13, 2019
McGregor akamatwa kwa kupora simu

Comments

comments