Rais Dkt. John Magufuli amthibitisha kaimu mkurugenzi wa taasisi na kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo kuwa mkurugenzi wa taasisi hiyo baada ya kuokoa bilioni 8.8 za wakulima.

Amefanya uamuzi huo baada ya kupokea ripoti kutoka ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) na  Takukuru Ikulu,, Chamwino jijini  Dododma leo Machi 26, 2020.

Amempongeza Mbungo kwa kazi nzuri ambayo anayofanya na inayofanywa na ntaasisi hiyo kwa ujumla japo amesema kuna watu wabaya wachache kwenye taasisi hiyo kama wa wilaya ya kinondoni na wenzake wanne.

”Nawapongeza Takukuru mmeweza kurudisha bilioni 8.8 za wananchi tena nafikiri Brig. Jenerali John Mbungo hautakiwi tu kuwa kaimu kuanzia leo wewe ni mkurugenzi mkuu takukuru kama umerudisha bilioni 8.8 basi utarudisha na mabilioni mengine ” amesema rais Magufuli.

Mbowe ajiweka karantini na familia yake
Magufuli ambana IGP " Serikali haiwezi kulipa mshahara waliokufa"

Comments

comments