Brigedia Marco Elisha Gaguti amemuagiza RPC Revocatus Malimi kuwakamata Mkandarasi wa Manispaa ya Bukoba na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kahororo kutokana na kutokukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo kwa Wakati

Pia, amegiza kukamatwa kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Mzinga Holding Company ambaye ni msimamizi wa ukarabati wa Shule Sekondari Kahororo na Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bukoba ambaye pia ukarabati wa Shule yake haujakamilika kwa wakati

Brigedia Gaguti amesema kuwa miradi hiyo kwa ujumla mpaka hivi sasa haifanyi vizuri na kutoa msisitizo kwa watu wanaoisimamia kukamilisha kwa wakati na muda uliopangwa pasipo kuomba muda wa nyongeza.

Waliokamatwa ni Mhandisi wa Manispaa ya Bukoba, George Geofrey; Mkandarasi wa Kampuni ya Mzinga Holding Company, Festo Tarimo; Mkuu wa Shule ya Sekondari Kahororo, Omary Ogambage pamoja na Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bukoba, Phocus Siasa.

Je, unatafuta ajira? hizi hapa nafasi za kazi kutoka makampuni 10 Tanzania
Bombardier Q400 ya Tanzania yakamatwa Canada, Profesa Kabudi afunguka