Baraza la mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), limeidhinisha jina la Mtanzania, Brigedia Jenerali Juma Nkangaa Sipe kuwa Mkurugenzi wa asasi ya siasa, ulinzi na usalama katika sekretarieti ya SADC.

Brigedia Jenerali, Juma Nkangaa Sipe anachukua nafasi ya Ukurugenzi wa asasi ya siasa, ulinzi na usalama katika sekretarieti ya SADC, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi asasi hiyo Jorge Kodoso kutoka Jamhuri ya Angola, kumaliza muda wake.

Akizungumzia hatua hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema suala la ulinzi na usalama katika Bara la Afrika, ni moja ya viapumbele vya Tanzania ili kutoa fursa biasahara kutokana na uwepo wa amani na hivyo kuiwezesha Afrika kupiga hatua za kimaendeleo

Kuhusu maendeleo ya mchakato wa Kiswahili kutumika kisheria katika vikao vya SADC, Mkurugenzi wa Jumuiya za Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Agness Kayola amesema, Tanzania tayari imewasilisha pendekezo la la kufanyiwa marekebisho kwa Mkabata wa uanzishwaji wa SADC.

Amesema, uwasilishwaji huo umefanyika ili kukitambua Kiswahili kisheria kama mojawapo ya lugha nne rasmi katika shughuli za SADC…….insert Balozi Agness Kayola,Mkurugenzi wa Jumuiya za Kikanda.

Ujumbe wa Tanzania, katika Mkutano wa kawaida wa 42 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), unatarajiwa kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye atawasili Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumanne ya Agosti 16,2022.

Rais Samia kuongoza Ujumbe wa Tanzania DRC
Kenya: Mgombea Urais akubali kushindwa