Pichani ni mashabiki pamoja na wachezaji wa Brighton & Hove Albion wakisherekea kwa furaha kufuatia timu hiyo kufanikiwa kurejea ligi kuu England baada ya kujaribu bila mafanikio kwa kipindi cha miaka 34.
Brighton & Hove Albion imerejea ligi kuu England baada ya  kuifunga Wigan Athletic kwa mabao 2-1 huko Amex Stadium jana jioni.
Shukrani kwa mabao ya Glenn Murray na Solly March.
Ushindi huo umeifanya Brighton & Hove Albion ifikishe alama (Point) 92. Alama saba mbele ya Newcastle United inayoshika nafasi ya pili na alama 13 mbele ya Reading inayoshika nafasi ya tatu. Timu zote zimebakiza michezo minne minne.
Brighton & Hove Albion ambayo mara yake ya mwisho kuonja radha ya daraja la ligi kuu ilikuwa ni msimu wa 1982-83 asa inahitaji kushinda mchezo wake wa Ijumaa ijayo dhidi ya Norwich City ili iweze kutawazwa bingwa wapya wa ligi daraja la kwanza nchini England.

Alexis Sanchez Kuuzwa Ufaransa?
Bondia Mada Maugo Ajidhulumu Ushindi