Nyota wa Singida Big Stars pamoja na kocha wa timu hiyo yenye maskani yake mkoani Singida, wameng’ara kwenye tuzo za mwezi Januari 2023 zinazotolewa na Bodi ya Liki Kuu Tanzania (TPLB).

Katika tuzo hizo Bruno Gomez amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Januari wa Ligi Kuu ya NBC kutokana na kiwango alichoonesha kilichotoa mchango mkubwa kwa timu yake na kuiwezesha kupata alama sita kwenye michezo miwili, huku akifunga magoli mawili.

Aidha, Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Pluijm amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Januari.
Pluijm amewashinda Robert Oliveira wa Simba SC na Nasreddine Nabi wa Young Africans alioingia nao fainali baada ya kuiongoza timu yake kushinda michezo miwili aliyocheza mwezi huo na kuendelea kushika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi.

Wakati huo huo, TPLB imemchagua Omary Malule ambaye ni Meneja wa Uwanja wa Highland Estates wa Ihefu FC kuwa Meneja Bora wa uwanja wa mwezi Januari 2023.

Omary amechaguliwa kutokana na kufanya vizuri katika usimamizi wa matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

SportPesa yamuibua Jemedari Said
SportPesa: Young Africans imekiuka makubaliano