Kampuni ya Bechmark Production inayoendesha shindano la Bongo Star Search (BSS) imeingia mikononi mwa Serikali baada ya kushindwa kutimiza ahadi iliyotoa kwa mshindi wa kwanza wa shindano la BSS 2019 la kutoa shilingi milioni 50 kwa Meshack Fukuta aliyeshinda katika shindano hilo.

Ambapo milioni 30 aliahidiwa kutumika katika kipindi cha mwaka mzima katika kumuendeleza kimuziki na kusimamia nyimbo atakazofanya ikiwa pamoja na video na sauti, huku milioni 20 kukabidhiwa kama pesa taslimu.

Taarifa hiyo imetolewa leo, leo April 8, 2020 na Naibu waziri wa habari, utamaduni sanaa na michezo Julina Shonza ambaye ametoa muda wa mwezi kwa viongozi wa shindano hilo kuhakikisha wamelipa kiasi hiko cha pesa walichoahidi kwa mshindi huyo.

Akizungumza Waziri ametamka Serikali haitasita kufungia shindano hilo la Bongo Star Search kwani wamekiuka sheria ya mashindano hayo ambayo inawataka mshindi akipatikana kulipwa siku hiyo ya shindano kinyume ambavyo wao wamefanya.

Mbali na aagizo hilo la kuwafungia, Waziri Shonza amewataka viongozi wa BSS kuripoti ofisini kwake na kuwasilisha mpango mkakati wa namna watakavyotumia milioni 30 waliyoahidi kuitumia katika kumuendeleza kimuziki katika kipindi cha mwaka mmoja.

Amesema hayo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea malalamiko kutoka katika familia ya Meshack ikieleza jinsi ambavyo wamesikitishwa na kitendo cha mtoto wao kutokulipwa fedha mara baada ya kushinda mashindani hayo.

”Mimi nilikuwa mgeni rasmi siku ya yale mashindano na mara baada ya mshindi kupatikani kulikuwa na sintofahamu katika eneo lile”amesema Shonza.

Aidha Serikali imeamua kuingilia kati baada ya jitihada kubwa zilizofanya na mshindi huyo pamoja na familia yake kugonga mwamba ndipo Serikali ilipoamua kuingilia kati baada ya kupokea malalamiko hayo toka kwa washtaki.

”Tulipokea barua ya malalamiko kutoka kwa familia au wazazi wa Meshaki kueleza nmna gani wao kama wazazi wamesikitika sana na wameuzunishwa sana kwa namna amabvyo kijana wao ametendewa” amesema Shonza.

Aidha Shindano la Bondo Star Search 2019 lilifanyika mnamo Disemba 24, 2019 jijini Dar es Saalaam katika ukumbi wa Next Door Arena, Naibu waziri Juliana Shonza akiwa kama mgeni rasmi wa shindano hilo ambalo Meshack aliibuka kidedea na kushika nafasi ya kwanza.

Serikali yazungumzia taarifa za wabunge 17 kukutwa na virusi vya corona – Kenya
BSS waagizwa kulipa milioni 50