Naibu Waziri Mhe.Juliana Shonza ametoa mwezi mmoja kwa uongozi wa Kampuni ya  Benchmark Production chini ya Mkurugenzi wake Madam Rita Paulsen  inayoendesha mashindano ya kusaka vipaji kwa wasanii wa muziki maarufu kama  Bongo Star Search (BSS) kuhakikisha wamemlipa mshindi  wa kwanza wa mashindano hayo ya mwaka 2019 kama walivyoahidi kutoa zawadi hiyo ya kiasi cha shilingi Milioni 50.

Mhe. Shonza ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kueleza umma jitihada ambazo serikali imefanya baada ya kupokea barua ya malalamiko ya kuto kulipwa kwa mshindi huyo kutoka kwa familia yao.

Kwa upande wa mshindi huyo wa mashindano hayo Bw.Meshack Fukuta  alisema mpaka sasa kampuni hiyo imemlipa kiasi cha shilingi milioni moja tu katika na siyo milioni mbili kama wanavyosema.

Pamoja na hayo Mhe.Shonza amewasisitiza wasanii kuhakikisha wanaandikishiana mikataba na watu mbalimbali wanaofanya nao kazi.

Mashindano hayo BSS yalifanyika Desemba 24, 2019 Jijini Dar es Salaam.

BSS hatarini kufungiwa, wapewa siku 30 kulipa milioni 50 za mshindi wa kwanza
Video: King Kiba avunja ukimya, aachia ngoma mpya ''Dodo'', Je amewatendea haki mashabiki?

Comments

comments