Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo, amesema kuwa hatagombea tena  nafasi ya Uenyekiti wa jumuiya  katika Uchguzi ujao.

Bulembo ameyasema hayo katika kikao cha Baraza hilo kilichofanyika mjini Dodoma na kutumia fursa hiyo kuwaaga wajumbe hao na kuwashukuru  kwa ushirikiano waliompa na kuweza kutekeleza majukumu yake.

“Naondoka katika nafasi hii nikiwa nimetekeleza ahadi zangu kwa asilimia 75 ambazo nilizitoa miaka mitano iliyopita wakati nikiwania nafasi hii katika Kampeni zangu, niliamua kuacha kazi zangu na kufanya kazi za jumuiya ambapo kwa sasa imebadilika, kwani siku ikuta hivi,”amesema Bulembo.

Amesema kuwa wajumbe wa jumuiya hiyo wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya jumuiya hiyo kujipima kwanza kama wanastahili kushika nafasi wanazoomba.

Aidha, Bulembo amewataka wanaotaka kugombea  nafasi za uongozi katika jumuiya hiyo wasimshirikishe kwa lolote, bali wakati ukifika wachukue fomu, atakutana na majina yao kwenye vikao vya maamuzi na si vingine.

Hata hivyo, baadhi ya wajumbe wa jumuiya hiyo wamepongeza hatua aliyoichukua Mwenyekiti huyo ya kutokugombea tena katika nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo.

Lwandamina Awakana Zanaco FC
Magazeti ya Tanzania leo Machi 10, 2017