Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amekiri kuwa kuondoka kwa Edward Lowassa kutoka katika chama hicho na kuhamia Chadema kuliwatikisa katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Akiongea katika mahojiano maalum na gazeti la Mwananchi, Bulembo alisema kuwa chama chao kilitikiswa na kishindo cha kuondoka kwa Lowassa kwa kuwa viongozi wengi wa chama hicho walikihama na kumfuata.

“Ukweli ni kwamba kuondoka kwa Lowassa kulitutikisa sisi CCM. Nasema CCM ilitikisika kwa sababu mbali na Lowassa tuliondokewa na wenyeviti watatu wa Mkoa wa Shinyanga, Singida na Arusha,” Bulembo alisema.

“Katika idara ya wazazi, mimi kama Mwenyekiti niliondokewa na wajumbe wa Baraza la mikoa ya Pwani, Kagera na Rukwa. Lakini tukapata replacement na kusonga mbele.

Baada ya Lowassa kuihama CCM, viongozi wengine wa ngazi za juu wa chama hicho walitangaza kukihama na kuweka historia katika siasa za Tanzania. Viongozi hao ni waziri mkuu mstaafu Frederick Sumaye na Kingunge Ngombale Mwiru ambaye ni mwanasiasa mkongwe zaidi wa chama hicho.

Hata hivyo, Bulembo alieleza kuwa waliweza kushinda uchaguzi huo kwakuwa mgombea wao wa urais, Dk. John Magufuli alikuwa anakubalika zaidi na aliweza kuongea ukweli majukwaani pamoja na ilani nzuri ya chama hicho.

Madereva wa Mabasi Ya 'Mwendo Kasi' wapanga kuigomea serikali
Van Gaal Agusia Jambo Dhidi Ya Pep Guardiola