Mkuu wa Idara ya Habari ya Young Africans Hassan Bumbuli, amejitosa kiaina kwenye mgogoro unaoendelea katika ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC Barbara Gonzales na Haji Manara.

Bumbuli amejiingiza kwenye gogoro hilo kwa kuandika maneno mafupi kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii mapema hii leo.

Hata hivyo Bumbuli ameonesha kushtukia kinachoendelea kwa wawili hao na kuuita mvutano wao ‘Maigizo’.

Bumbuli ameandika “Ndugu wakigombana, Shika Jembe Ukalime.
Sisi Majembe yametua Kigoma, hayo maigizo tumewaachia wenyewe.”

Tayari kikosi cha Young Africans kimeshaanza safari ya kuelekea Kigoma, kwa ajili ya mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba SC utakaochezwa Jumapili (Julai 25), Uwanja wa Lake Tanganyika.

Barbara: Sio muda sahihi kumjibu Manara
PICHA: Young Africans yatangulia Kigoma