Vinara wa Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/22 Young Africans wametamba kuendeleza ubabe dhidi ya Watani zao wa Jadi Simba SC, Jumamosi (Desemba 11) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Young Africans ambayo inatakua Mgeni katika mchezo huo imetamba kupitia idara yake ya Habari na Mawasilino inayoongozwana Hassan Bumbuli.

Bumbuli ametoa tambo hizo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Makao Makuu ya Shirikisho la soka nchini Tanzania ‘TFF’ leo mchana, huku akisema kikosi chao kipo tayari kwenda kuendeleza ubabe kama kilivyofanya kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii mwezi Septemba.

Katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Young Africans iliibuka na ushindi wa 1-0, likifungwa na Mshambuliaji kutoka DR Congo Fiston Kalala Mayele.

“Tumejiandaa kushinda mchezo huo, mpaka sasa kikosi chetu kipo vizuri na hadi nakuja hapa taarifa nilizozipata kutoka kambini wachezaji wote wapo katika hali nzuri isipokua Yacoub Sogne, ambaye ni Majeruhi,”

“Dhamira yetu ni kupata matokeo ambayo yatatuongezea nafasi ya kulisogelea Taji la Ligi Kuu ambalo tumelikosa kwa muda mrefu, tunaamini msimu huu Taji hili lina kila sababu ya kurudi nyumbani.” amesema Bumbuli

Young Africans inaelekea kwenye mchezo huo ikiwa inongoza Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 19, huku Simba SC ikiwa nafasi ya Pili kwa kufikisha alama 17.

Simba SC yatamba kuongoza Msimamo Jumamosi
Ndege inayoruhusu mambo ya faragha kufanyika angani