Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Young Africans Hassan Bumbuli, amewataka Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo kuendeleza Shangwe, baada ya kumfunga Mnyama Jumamosi (Julai 03).

Bumbuli amesema Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo hawana budi kushangili kutokana na maneno ya kebehi yaliyosemwa kabla ya mchezo wa Jumamosi.

Amesema Young Africans walidhaurika na kuonekana hawana wachezaji kama ilivyo kwa watani zao Simba SC, ambao walishindwa kufurukuta ndani ya dakika 90.

Mbali na hilo, Bumbuli anaamini Young Africans ina nafasi nyingine ya kuifunga Simba SC kwenye mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) utakaochezwa Julai 25, mjini Kigoma Uwanja wa Lake Tanganyika.

“Tutawafunga tena Simba, Kama wameshindwa kutufunga Dar wakiwa na Chama, Luis na Morrison, kule Kigoma watamuongeza mchezaji gani..?” amehoji Bumbuli

“Tutawaalika Simba siku ya Mwananchi ili tuwafunge, tutawaomba na kwenye Simba day tukacheze nao ili tuwafunge wakikataa tunaenda hivyo hivyo kuwafunga.” amesema Bumbuli.

Licha ya kuifunga Simba SC, Young Africans ina matumaini hafifu ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, lakini ina nafasi ya kutwaa taji la Kombe la Shirikisho (ASFC).

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 7, 2021
Kenneth Muguna kutua Jangwani