Klabu za igi kuu nchini Ujerumani (Bundesliga) zimeendelea kutoa heshima ya kifo cha Mmarekani mweusi Floyd aliyepoteza maisha baada ya kubanwa shingo, kwa kuvalia nguo au ishara ya kupinga tukio hilo.

Maandamano ya amani yaliyokuwa na ujumbe Black Lives Matter yameendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii huku watu mashuhuri wakihanikiza tukio hilo la kinyama, Paul Pogba, Serena Williams, Lewis Hamilton, wakiwa ni miongoni mwa watu walioandika ujumbe kuhusu tukio hilo.

Timu ya Borussia Dortmund ikiwa imevalia jezi za mazoezi zenye ujumbe wa kuhimiza amani, haki na umoja na Hertha Berlin walipiga magoti katikati ya duara la Signal Iduna Park kabla mtanange baina ya timu hizo kuanza ikiwa ni sehemu ya kuungana na ulimwengui kupinga ukatalii.

Wachezaji wa Bayern Munich pia walivalia “Flana” zilizokuwa zikipinga ubaguzi wa rangi kabla ya mchezo ulioishuhudia Bayern Munich ikiibuka na ushindi wa goli 4-2 dhidi ya Bayer Leverkusen.

Kwa siku za hivi karibuni, upingwaji wa ubaguzi dhidi ya mauaji ya George Floyd umeibuka na kutetewa kwa kiasi kikubwa na kupewa kipaumbele na watu wa kada tofauti tofauti.

Azam FC watuma mwaliko KMC FC
Serikali kutoweka bei elekezi zao la Pamba