Bunge nchini Tunisia limepiga kura ya kuidhinisha serikali mpya, itakayoanza kutekeleza majukumu yake siku chache zijazo.

Serikali ya umoja inayoongozwa na waziri mkuu, Youssef Chahed, iliungwa mkono na wabunge 167, kati ya wabunge 217.

Serikali ya bwana Chahed inashirikisha wahafidhina wa kiislamu, wanasiasa wa mrengo wa kushoto, wanaharakati wa vyama vya wafanyakazi na wanasiasa binafsi.

Bwana Chahed ameahidi kuchukua hatua dhabiti za kuimarisha uchumi wa taifa hilo pamoja na usalama.

Youssef Chahed, 40, ameweka historia katika taifa hilo kwa kuwa waziri mkuu mwenye  umri mdogo sana tangu taifa hilo lipate uhuru wake kutoka kwa Ufaransa, mwaka 1956.                                                                                                                                                                                                                                       Youssef Chahed, aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya Tunisia aliteuliwa kuwa waziri mkuu baada ya  kuondolewa kwa waziri mkuu aliyepita kwa kura ya kutokuwa na imani nae mwezi uliopita

Uchaguzi Wa Urais Waanza Gabon
Video Mpya: Mo Music - Ado Ado