Raisi wa Venezuela Nicolas Maduro anamtambua Luis Parra kama mrithi wa Juan Guaido kwenye kiti cha uspika kwakuwa Guaido ameondolewa na kura za wapinzani wenzake.

Juan Guaido amabye ni mpinzani wa Rais wa Venezuela amechaguliwa tena kuwa Spika wa Bunge na Wabunge wa Upinzani saa chache baada ya Mbunge mwingine wa upinzani, Luis Parra, kujitangaza kuwa Spika wa Bunge hilo.

Luis Parra, amejitangaza kuwa Spika wa Bunge katika kikao ambacho Juan Guaido na Wabunge wengi wa upinzani hawakuweza kuhudhuria baada ya kuzuiliwa nje ya jengo hilo kwa muda mrefu na Polisi.

Guaido alichaguliwa na wabunge wapatao 100 wakiwemo wengine kadhaa ambao walilazimika kukimbilia uhamishoni mwaka jana kutokana ana ukandamizaji wa serikali ya Maduro.

Upinzani unaomuunga mkono Guaido, ambaye nchi zaidi ya 50 zinamtambua kama Rais wa mpito wa Venezuela huku Luis Parra ambaye amekula kiapo bila ya kuchaguliwa na idadi ya wabunge iliyokamilika na kwa hilo amefanya Mapinduzi ya Bunge.

CAG: Awawasha wadaiwa sugu Bodi ya Mikopo
Harmonize , Waitara wachafua hewa CCM, Kidato cha kwanza kurundikana miezi miwili