Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeanza jana mjini Dodoma na moto ambao wengi waliutabiri huku harufu ya ushabiki wa vyama ikitawala.

Katika zoezi la kumtafuta Spika wa Bunge hilo lililotanguliwa na maswali na majibu kwa wagombea nane waliojitokeza, Mgombea Uspika kupitia Chadema, Goodluck ole Medeye alikwaruzana kimtazamo na mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye.

Swali la Nape lililokuwa kati ya maswali matatu aliyoulizwa Ole Medeye lilionekana kumuudhi mgombea huyo. Nape alimtaka Ole aeleze kama ameacha tabia ya ubaguzi kwa madai kuwa Godbless Lema aliwahi kumtuhumu kuwa ni mbaguzi.

Ingawa Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Andrew Chenge alikataa swali hilo lisijibiwe akieleza kuwa halikuwa swali, Ole Medeye alihitimisha kwa kumueleza Nape alichokuwa nacho moyoni ingawa hakumtaja jina.

“Kuna mbunge hapa aliniuliza swali ambalo kwa lugha za kibunge tunaliita ni swali la kuudhi. Mbunge huyo nimemsamehe, sina chuki naye kwa sababu najua kinachomsumbua ni utoto tu, akikua ataacha,” alisema Ole Mideye.

Uchaguzi huo ulikamilika na kumuwezesha Job Ndugai kuwa spika wa Bunge hilo baada ya kupata asilimia 70 ya kura zote.

Video: Angalia Algeria Ilivyoituliza Taifa Stars Jana
Lionel Messi Ameanza Mdogo Mdogo