Bunge la Peru limemuondoa madarakani Rais Pedro Castillo na nafasi yake kuzibwa na makamu wake, Dina Boluarte muda mfupi baada ya Castillo kujaribu kulivunja bunge hilo, ikiwa ni kabla ya zoezi la kumpigia kura ya kumwondoa.

Ofisi maalumu inayohusika na masuala ya uchunguzi nchini humo imesema, kitendo cha Castillo kinahusishwa na kupoteza udalifu kazini kwa kujairibu kulivunja bunge kitu ambacho ni sawa na tukio la mapinduzi.

Rais aliyeondolewa madarakani, Pedro Castillo. Picha ya BBC.

Katika tukio hilo, kura za ndio zilikuwa 101 na za hapana 6 huku kura 10 zikiharibika na muda mfupi kabla ya kupigwa kwa kura hizo Castillo alitangaza kuweka Serikali ya dharura na kutaka duru ya pili ya mkutano wa bunge ya kufanikisha katiba mpya taifa hilo.

Serikali ya Marekani imesema imeupokea uteuzi wa Boluarte kama Rais wa Peru, ambaye tayari ameapishwa na bunge la taifa hilo katika siku ambayo Castillo akitiwa nguvuni baada ya kuondolewa madarakani.

Rais mpya wa Peru, Dina Boluarte. Picha ya BBC.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imepongeza umadhubuti wa taasisi za Peru kwa kuhakikisha demokrasia inaimarika na itaendelea kuliunga mkono taifa hilo chini ya serikali ya umoja wa kitaifa.

Boluarte, mwanasheria mwenye umri wa miaka 60, atakuwa mwanamke wa kwanza kufikia ngazi ya urais nchini Peru, tangu ipate uhuru wake zaidi ya miaka 200 iliyopita.

Mauaji ya Mwandishi Kenya yalipangwa: Ripoti
Aliyeuwa mke na mtoto ahukumiwa kunyongwa