Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wabunge wake, leo Juni 26, 2018 limepitisha kwa kishindo makadirio ya fedha kwa mwaka 2018/ 2019 ya Sh 32.45 trilioni.

Ambapo wabunge waliopiga kura ni 348, wabunge 266 wamepitisha bajeti hiyo kwa kura za ndiyo huku wabunge 82 wamepiga kura za hapana, na hakuna kura yeyote iliyoharibika.

Wabunge 43 hawajaweza kupiga kura kutokana na kutokuwepo bungeni, akiwemo kiongozi wa kambi kuu ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe.

”Mheshimiwa Spika Idadi ya wabunge waliopo na walioiga kura walikuwa 348, na wabunge ambapo hawakwepo bungeni walikuwa 83, kura za hapana zilikuwa 82, hakuna kura ambayo haikuamua nakura za ndio zilikwepo 266” amesema Katibu ambaye alitangaza matokeo ya kura za makadirio ya fedha mwaka 2018/2019.

Wabunge Hussein Bashe, Nape Nnauye na Abdalah Bulembo (CCM) wameshangiliwa zaidi bungeni kwa kupiga kura ya ndiyo, kutokana na hoja mbalimbali walizokuwa wanazijenga bungeni.

Aidha  Bunge LImepitisha muswada wa sheria kuidhinisha matumizi ya serikali…, Bofya hapa kutazama Video.

Simba yamsajili Meddie Kagere kwa dau hili
LIVE: Wabunge wakipigia kura Bajeti Kuu ya Serikali 2018/19

Comments

comments