Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson amesema hakuna Mbunge aliyejiandikisha kuuliza maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Alhamisi Mei 6, 2021.

Dkt Tulia ametoa ufafanuzi huo leo baada ya kuanza kwa kipindi cha maswali na majibu bungeni.

Ni utaratibu wa Bunge kila Alhamisi wabunge hupata nafasi ya kumuuliza Waziri Mkuu maswali ya papo kwa hapo kwa dakika zisizozidi 30.

Hata hivyo wakati Naibu Spika akisema hayo, ndani ya ukumbi wa bunge Majaliwa hakuwepo na haikuelezwa nani anayekaimu nafasi yake leo.

Rais Samia kukutana na wazee Dar
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 6, 2021