Bunge la Senate jana lilimpa ushindi Donald Trump baada ya kupitisha kwa kura jina alilolipendekeza kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Bunge hilo la Senate lilimuunga mkono Trump kwa kura 50 dhidi ya 48, baada ya mjadala na mvutano wa siku kadhaa kuhusu tuhuma za unyanyasaji wa kingono zilizoibuliwa dhidi ya mteule huyo, Brett Kavanaugh (anayeapishwa pichani).

Hata hivyo, Kavanaugh alipinga vikali tuhuma hizo akieleza kuwa zimepikwa kisiasa. Uchunguzi uliofanywa na FBI ulitosha kuwashawishi wabunge wengi kumuunga mkono.

Kupitishwa kwa jina hilo kumeandika historia ya ushindi kwa Trump ambayo inampa mwanga mpya kuelekea chaguzi ndogo za Novemba.

Kabla ya upigaji kura huo, mamia ya watu waliandamana katika mitaa ya jiji la Washington kupinga uteuzi wa Kavanaugh.

Aidha, ushindi huo uliibua kelele ndani ya nyumba hiyo ya wawakilishi ambapo wapinzani walipiga kelele kuu, “aibu yenu”, hali iliyomlazimu Makamu wa Rais, Mike Pence kuingilia kati na kuomba amri ya utulivu izingatiwe.

Kavanaugh ameapishwa kuwa Jaji mwenye mkataba wa kuitumikia nafasi yake katika kipindi cha maisha, huku akiwa kwenye Mahakama inayofanya uamuzi wa mwisho nchini humo.

Sanchez asimika ‘mkuki’ kumlinda Mourinho, afunguka
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 7, 2018