Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewahakikisha waaumini wa dini ya Kiislamu kuwa watahakikisha upatikanaji wa mafuta na Tende unakuwa wa kutosha pamoja na kuwepo bei nzuri ili waweze kula vyakula vya mafuta kwa wingi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani utakaoanza hivi karibuni.

Hayo yamesemwa hii leo bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe, aliyetaka kusikia kauli ya serikali juu ya kuangalia uwezekano wa kufuta kodi katika uingizaji wa Tende nchini kutokana na kuwa zao hilo linatumika kwa kiasi kikubwa ndani ya mwezi wa Ramandani unaotarajiwa kuanza ndani ya mwezi huu pamoja na bei ya mafuta ya kula na sukari kuwa juu kwa kipindi kifupi.

“Sasa hivi kwenye hifadhi ya matenki Dar es Salaam kuna CPO takribani tani 40,000 na meli zilizopo nje zina CPO tani 50,000. Kinacholeta tatizo ni kutokubaliana katika viwango vya kodi maana ukileta mafuta kwa sheria tuliyopitisha sisi watanzania tunamtoza muagizaji asilimia 10,”amesema Mwijage

Aidha, amesema kuwa suala la Tende ni jambo la kwenda kuzungumza na Waziri wa Fedha ili kuona namna ya kuweza kushughulika nalo.

Hata hivyo, Mwijage ameongeza kuwa atalishughulikia suala la kodi la uingizaji mafuta ili iweze kufahamika kama ni asilimia 10 inapaswa kutozwa na serikali au asilimia 25.

 

 

Bodi ya Mikopo yavuka malengo ya ukusanyaji madeni
Bei mafuta ya kula yapaa