Kampuni za simu, ambazo zimekuwa zikitoa huduma zenye kasi ndogo zimetakiwa kuwafidia wananchi kutokana na biashara inayoendelea kati ya Kampuni hizo na wateja.

Madai hayo, yametolewa hii leo Februari 6, 2023 na Mbunge wa jimbo wa Ulyankulu (CCM), Rehema Migilla wakati akiuliza swali la nyongeza na kusema huduma hizo ni biashara na mwananchi anapotoa fedha huhitaji huduma nzuri.

Minara ya Mawasiliano.

Amesema, kutokana na kasi ndogo ya minara katika eneo la jimbo lake vifurushi vya huduma huisha muda wake bila kutumika na kusema, “hizi kampuni za simu ziko tayari kuwafidia hawa wananchi wetu ambao fedha zao zimetumika bila kupata huduma kwa sababu huu ni wizi kama wizi mwingine,”

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Methew Kundo akijibu swali hilo amesea minara iliyopo katika maeneo hayo katika kata ya Nhwande inauwezo wa 2G pekee na upo mpango ni kuiboresha ili kufikia 3G hadi 4G.

Zaidi ya 500 wafariki kwa tetemeko la ardhi
Young Africans yawashtukia waarabu Dar