Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa (JKT), Dkt. Stergomena Tax amesema hakuna mpango wa kubadili utaratibu wa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wa kukaa miaka sita bila kuoa ama kuolewa, mara baada ya kujiunga na jeshi hilo.

Dkt. Stergomena, ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa jimbo la Bunda, Boniface Getere aliyetaka kupunguzwa kwa miaka sita iliyopo kwa askari wapya wa Jeshi kuoa ama kuolewa, na kuwa mwaka mmoja ama miaka miwili.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa (JKT), Dkt. Stergomena Tax.

Akijibu suala hilo, Waziri huyo wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa (JKT), amesema kuwa kwa sasa utaratibu huo utabakia kama ulivyo, kutokana na misingi iliyowekwa kwa ajili ya kuwaandaa askari hao kulinda nchi, hivyo utapaswa kufuatwa kama ulivyo.

Ameongeza kuwa, askari wapya wanaojiunga na Jeshi wanahesabiwa kama wapiganaji ambao wanapaswa kupewa ujuzi zaidi na kutumika kwenye vita, hivyo miaka sita iliyowekwa ya kutokuoa ama kuolewa inatoa nafasi kwa askari hao, kutumika katika shughuli za medani.

Puttin apata 'kigugumizi' usaidizi wa china kwa Urusi
Kocha Zalan FC awahofia Fei Toto, Mayele