Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amesema, muswada wa Bima ya Afya kwa Wote (UHC), uliokuwa uwasilishwe Bungeni hii leo Februari 9, 2023 umeshindikana tena, kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya mambo katika utekelezaji wake.

Dkt. Tulia amesema, muswada huo ambao ulikuwa uanze kujadiliwa bungeni leo na kesho Februari 9-10, 2023 umerejeshwa kwenye kamati kwa ajili ya kujadiliwa zaidi na kisha utapelekwa Bungeni baadaye.

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson.

Amesema, baada ya muswada wa Bima ya Afya kwa Wote kusogezwa mbele kwa sasa majadiliano yanaendelea na hasa eneo la bajeti na utekelezaji wake.

Muswada huo, unakwama kwa mara ya pili tangu usomwe kwa mara ya kwanza bungeni katika mkutano wa nane wa Bunge na kupelekwa katika kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kujadiliwa.

Watumishi 12 mbaroni kwa kuvujisha mitihani
Tetemeko la ardhi latikisa Tanzania, Kenya