Beki wa zamani wa Luton Town ya Uingereza ambaye amewahi kuvinoa vilabu vya Real Madrid, Atletico Madrid na Barcelona, Radomir Antic, amefariki leo akiwa na umri wa miaka 71.

Alijiunga na Luton mwaka 1980 akiichezea zaidi ya mechi 100 na atakumbukwa zaidi kwa bao lililowashusha daraja Manchester City msimu wa 1982/83 katika mechi ya kihistoria iliyopigwa Mei 14. 1983 wakishinda 0-1 na kusalia Ligi Daraja la Kwanza enzi hizo (Sasa EPL).

Amezifundisha timu kadhaa barani Ulaya hasa Hispania zikiwemo Real Zaragoza (1988-1990), Real Madrid (1991-1992), Atletico Madrid (1995-1998, 1999 na 2000), Barcelona (2003), Celta Vigo (2004), na timu ya taifa ya Serbia mwaka 1998-2000.

Mafanikio yake makubwa kama kocha aliyapata katika msimu wa 1995-96 akiwa na Atletico Madrid ambako alitwaa ubingwa wa LaLiga na Copa Del Rey.

Ni raia wa Serbia ambaye alikuwa akiitumikia timu ya taifa ya Yugoslavia na ni kocha wa pili kuzinoa timu zote mbili zenye uhasama mkubwa nchini Hispania, Real Madrid na Barcelona.

CAG aianika Wizara ya Maliasili, 'Sh 2.5 bilioni zilitumika bila utaratibu'
Mfumo mpya Young Africans kukamilika mwezi ujao

Comments

comments