Mshindi wa Tuzo ya Grammy na mwanamuziki mahiri kutoka nchini Nigeria Damini Ebunoluwa Ogulu, maarufu Burna Boy, amejipatia zawadi ya gari la kifahari aina ya Lamborgin Urus ya mwaka 2022 yenye thamani ya dola 608K ambazo ni zaidi ya Bilioni 1.3 za kitanzania.

Toleo hilo la Urus Novitec ni miongoni mwa matoleo ghali ya Novitec Group yaliyotengenezwa kwa ubora zaidi miongini mwa magari yanayozalishwa na kampuni hiyo.

Burna Boy alitumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuonyesha gari hilo akiambatanisha na ujumbe mfupi uliosomeka.

“KRISMASI NJEMA NA HERI YA MWAKA MPYA DAMINI. MUNGU ANAKUPENDA, FAMILIA YAKO INAKUPENDA NA MIMI NAKUPENDA. HUTAHITAJI KITU KINGINE.”

Nyoka wa kichawi asimamisha mradi wa Sh. 99 bilioni Tanga
Kenya yapiga marufuku kutembea usiku