Moja ya vitu vinavyo dhihirisha ukubwa wa msanii ni pamoja na namna anavyoweza kuhamasisha mashabiki zake kufuata jambo analolianzisha au analoliihitaji msanii kutoka kwao na wakafanya hasa akiwa nje ya nchi yao.

Msanii kutoka Nigeria Damini Ebunoluwa Ogulu, maarufu kama Burna Boy amelizihirisha hilo usiku wa kuamkia leo Agosti 28, 20021 baada ya kuweka rekodi ya kipekee, kwa kuwa mmoja wa wasanii wa Afrika aliyeweza kupata idadi kubwa zaidi ya mshabiki kwenye tamasha lake lililofanyika kwenye moja ya Arena kubwa na maarufu sana dunia #O2 iliyoko huko London.

Inaelezwa kuwa msanii Burna ameweza kuwakusanya watu zaidi ya elfu ishirini (20) waliijitokeza kutazama show hiyo katika ukumbi huo wa O2 huko london.

Burna Boy hivi karibu ameonekana kuzidi kuzisogelea nafasi za juu zaidi kwenye orodha ya wasanii wa Afrika wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani, ambaye mpaka sasa ni mmiliki wa tuzo mbali mbali za kimataifa ikiwemo GRAMMY aliyoshinda kupitia album yake Twise as Tall, pamoja na BET aliyoipata kupitia kipengele cha best International act mwaka 2021 huko nchini Marekani.

Oman yaondoka katazo kwa abiria kutoka Tanzania kuingia nchini humo
Jeshi la Polisi lamaliza uchunguzi mwili wa Hamza