Mahakama ya Katiba nchi Burundi imeagiza kutawazwa kwa rais mteule, Jenerali Evariste Ndayishimiye baada ya kifo cha Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza kilichotokea wiki hii.

Agizo hilo la Mahakama ya Katiba inamaliza sintofahamu iliyokuepo kuhusu nana atakaye chukuwa nafasi ya Rais baada ya Rais Pierre Nkurunziza kufariki dunia ghafla Jumatatu Juni 8 kuokana na shinikizo la moyO, kwa mujibu wa serikali ya Burundi.

“hakuna ulazima wa kuwepo na Rais wa mpito”. Hoja kuu ya Mahakama ni kuzingatia kwamba madhumuni ya serikali ya mpito ambayo ni kuandaa uchaguzi wa mapema iwapo kutakuwa na ombwe la uongozi nchini hoja ambayo haipo tena nchini Burundi, baada ya kuepo na rais mteule.” Imeeleza taarifa kutoka Mahakama hiyo

Wakati huo huo, Mahakama ya Katiba imeagiza kwamba Jenerali Evariste Ndayishimiye aapishwe haraka iwezekanavyo, ili kuchukuwa hatamu ya uongozi wa nchi.

Ndayishimiye wa chama tawala cha CNDD-FDD aliyechaguliwa Mei 20 awali ilikuwa aapishwe mwezi Agosti.

Bwana Ndayishimiye ni miongoni mwa waliokuwa waasi wa CNDD-FDD waliojiunga na kundi hilo baada ya kunusurika katika mauaji ya kikabila ya wanafunzi Wahutu katika chuo kikuu cha Burundi mwaka 1995, kufuatia mauaji ya rais Melchior Ndadaye mnamo mwaka wa 1993.

Yaliyojiri simu ya Magufuli kwa Rais Mpya wa Burundi
Msajili ampa Zitto siku saba, Kikao na Balozi wa Uingereza champonza