Chama kikuu cha upinzani nchini Burundi, CNL kimesema kitayapinga mahakamani matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo jana Jumatatu, yaliyompa ushindi mgombea wa chama tawala cha CNDD/FDD, Evariste Ndayishimiye.

Msemaji wa CNL Therence Manirambona amesema chama chake kimesusia mkutano wa kuyatangaza matokeo hayo ya awali, kwa sababu ingekuwa kuunga mkono alichokiita ”kiloja” na kurudia shutuma kwamba shughuli ya uchaguzi wa Jumatano iliyopita pamoja na ya kuhesabu kura zilikumbwa na mizengwe.

Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa na jana na tume ya uchaguzi mjini Bujumbura, mgombea wa chama cha CNDD/FDD ameshinda kwa asilimia 68.72, akifuatiwa na Agathon Rwasa wa CNL aliyeambulia asilimia 24.19. Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa na korti ya katiba tarehe nne mwezi Juni.

Jeshi la Polisi: Idris Sultan alijaribu kuharibu ushahidi
Kenya: Familia 600 zakosa makazi kutokana na mafuriko