Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Burundi, Pierre-Claver Kazihise, ametoa wito kwa wananchi kuwa na subira, huku masanduku ya kura yakiwa yanaendelea kukusanywa na kura zikiwa zinahesabiwa.

Kazihise aliwasihi watu kuwa na utulivu, akisema mchakato wa kuhesabu kura zote utachukua siku kadhaa, na matokeo yatatangazwa Jumatatu au Jumanne.

Kufuatia kampeni zilizogubikwa na vurugu, uchaguzi ulikuwa shwari uliokuwa na ushindani mkubwa utakaoamua mrithi wa kiongozi wa muda mrefu nchini humo Pierre Nkurunziza.

Hata hivyo kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha National Freedom Council (CNL), Agathon Rwasa amedai kulifanyika udanganyifu katika uchaguzi huo na maafisa wake kadhaa walikamatwa.

Tume ya uchaguzi bado haikujibu madai hayo. Uchaguzi uliopita wa mwaka 2015 uliompa ushindi wa muhula wa tatu Nkurunziza, ulisababisha vurugu zilizopelekea watu 1,200 kuuawa na wengine wapatao 400,000 kuikimbia nchi.

Wahudumu wa afya 10,000 waambukizwa corona Iran
Dk. Abbas: Timu zianze mazoezi