Viongozi wa Kiislamu nchini Burundi wamejitenga na kauli iliyotolewa na mmoja wao kwa kumkosoa Waziri wa Mambo ya Ndani aliyetoa wito kwa mashekhe kupunguza sauti ya adhana ya asubuhi ili isiwe kero kwa umma.

Kwa mujibu wa shirika lahabari la BBC, Waziri wa Mambo ya ndani wa Burundi Gervais Ndirakobuca katika kikao cha pamoja na viongozi kidini aliwaomba wasipige kelele wakati wa maombi ya usiku na kwa wenzao wa Kiislamu kupunguza sauti ya Adhana (wito wa sala) wakati wa alfajiri.

Sheikh Ndikumana Rashid, alisikika akimkaripia Waziri na kumtaka afutilie mbali matamshi aliyotoa na kuomba msamaha.

Sheikh Rashid alisema kauli ya waziri ni shambulio la moja kwa moja dhidi ya dini ya Kiislamu.

Wawakilishi wa Waislamu hata hivyo wamesema Rashid atawajibikia kauli yake kwa kumtukana waziri.

Mkuu wa Baraza la Waislamu nchini Burundi Zuberi Mohamed, amesema hakuna mzozo kati ya Waislamu na serikali akiongeza kuwa wito wa sala jimbo la kawaida.

Rais Samia awasili Mwanza kwa ziara ya siku tatu
Aliyerekodi tukio la kuuawa George Floyd apewa tuzo