Wananchi wa Burundi leo Alhamisi Mei 17, 2018 wanapiga kura ya maoni kwa kufanya marekebisho katika nchi hiyo ili kuongeza muda wa Rais kubakia madarakani kutoka miaka mitano ya sasa hadi saba.

Endapo marekebisho hayo ya katiba yakiidhinishwa na wananchi huenda, Rais Pierre Nkurunziza akaongoza taifa hilo hadi mwaka  2034,

Licha ya kampeni hizo kuchafuliwa na tishio za upinzani kususia kura hiyo kwa madai ya serikali kuwatisha wafuasi wa upinzani.

Rais Pierre Nkurunziza amekuwa akipiga kampeni nchini humo, akiwaeleza wananchi kuwa katiba hiyo mpya ni ya manufaa kwao, lakini wanaopinga wanamwona kama mwenye tamaa ya madaraka wakati Serikali ikikanusha madai hayo na kusema mabadiliko yanayopendekezwa ni ya kuboresha katiba.

Burundi imebadilisha katiba yake mara kadhaa miaka ya hivi punde ambapo miaka mitatu iliyopita Nkurunziza alifanikiwa kujiongezea muda zaidi ya miaka kumi iliyotarajiwa, hali ambayo ilileta maandamano yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 700 huku wengine wapatao 400,000 wakitoroka makwao baada ya msako wa serikali.

Wapinzani wanamshutumu Rais huyo kwa kupuuza makubaliano yaliyoafikiwa jijini Arusha, ambayo yaliweka ukomo muda wa rais kuwa madarakani usizidi miaka kumi. Lakini mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yakielezea wasiwasi wao na kusema wapinzani wamekuwa wakishambuliwa.

Serikali imekanusha vikali madai haya, ikieleza kuwa wapinzani wa kura hii wamepewa fursa ya kufanya kampeni zao kwa njia iliyo huru licha ya taharuki kutanda nchini humo na baadhi ya viongozi wa upinzani kutorokea nchi nyingine.

Gianluigi Buffon atangaza kuondoka Juventus
Makala: Trump na Kim Jong-un, Mtego wa ndege mjanja na tundu bovu